Kagame ametaja wakati atakapoonyesha upande wake kuhusu kuwania awamu nyingine

Rais Kagame Paul amesema atatangaza msimamo wake kuhusu kugombea urais tena mwaka 2017, baada ya kura ya maoni.

Alipokuwa katika mkutano wa viongozi wa Chama chake RPF Jumapili hii, rais Kagame alisema hawezi kuonyesha msimamo wake kabla ya kura ya maoni.

Rais ameendelea kusema jibu lake litazingatia yatakayokuwa ametoka ndani ya kura ya maoni.

"Jibu mnalolitaka kwangu, litatokana na matokeo ya kura ya maoni. Siwezi kujibu kabla.Ni lazima kuchunguza vizuri yatakayotokea kutokana na uchaguzi wetu au kutafuta njia nyingine." alisema Kagame

Marekani na Umoja wa Ulaya wamepinga hatua ya bunge ya Rwanda ya kurekebisha katiba ili rais Kagame apate kuwania awamu nyingine.

Mke wake rais Kagame (kati) katika mkutano wa chama tawala RPF

Bunge limesema ni kutokana na maombi ya raia wanaotaka waendelee kuongozwa na Kagame.

Hata hivyo, Kagame amesisitiza uamuzi wa wanyarwanda ni haki yao bila kulazimishwa na yeyote.

"Kila siku wanatufundisha kujichagulia, lakini tukichagua, inaonekana ni kulazimisha bunge ya kufanya ? mbona wanatulazimisha kuishi namna wanavyotaka ? vipi chaguo letu ni tatizo linalowahusu wengine ? aliuliza Kagame

wanachama wakuu wa RPF

Katika mkutano huo wa viongozi wa RPF, wamemuomba Kagame aweke tarehe ya kura ya maoni.

Kagame amewaomba wamusaidie kuweka tarehe hiyo, na kupendekeza ifanyike tarehe 18 Desemba.

Tarehe hiyo itachunguzwa na baraza la mawaziri wiki hii, baadaye itangazwe .

Ferdinand Maniraguha

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments