Rais Kagame apandisha vyeo zaidi ya wanajeshi 5000

Wakati Rais Kagame alipopandisha maafisa wakuu 528 mwezi Juni 2015

Rais wa Rwanda Paul Kagame akiwa pia amiri jeshi mkuu wa majeshi ya Rwanda, amepandisha vyeo wanajeshi 5726 wakiwemo 10 waliopewa cheo cha Brigadier General, 46 wamepewa cheo cha Kanali huku wengine 182 wakipewa cheo cha Luteni Kanali

Kulingana na tangazo lililotolewa na wizara ya ulinzi, wanajeshi waliopandishwa ni hawa wafuatao :

Waliokuwa na cheo cha Kanali wamepandishwa cheo cha Brigadier General ni

(1) Col John Gashaija Bagirigomwa
(2) Col Emmanuel Ndahiro
(3) Col Denis Rutaha
(4) Col Ephrem Rurangwa
(5) Col Eugene Nkubito
(6) Col Jean Damascene Sekamana
(7) Col Chris Murari
(8) Col Didas Ndahiro
(9) Col Firmin Bayingana
(10) Col Evariste Murenzi

Wanajeshi 46 waliokuwa na cheo cha Luteni Kanali wamepewa cheo cha Kanali

wanajeshi 182 waliokuwa na cheo cha meja wamepewa Luteni Kanali

Wanajeshi 685 waliokuwa Captain wamepewa cheo cha Major

Wengine 1018 waliokuwa Luteni wamepewa Captain

Wanne waliokuwa usu luteni wamepewa Captain

Watatu waliokuwa madaktari (Medical Doctors) wamepewa cheo cha Captain

Wawili waliokuwa luteni usu (Second Lieutenant) wamepewa cheo cha Luteni

Saba waliokuwa na cheo cha sergeant wamepewa cheo cha Sergeant Major wengine wakapewa cheo cha Warrant Officer Two

Wanajeshi 39 walikuwa Staff Sergeants wamepewa cheo cha Sergeant Major
Sergeant 1 kapewa Sergeant Major

Wengine 20 waliokuwa na cheo cha Sergeant wamepewa cheo cha Staff Sergeant

Askari wengine 272 waliokuwa na cheo cha Corporal wamepewa cheo cha Sergeant

Askari 3437 waliokuwa na cheo cha Private wamepewa Corporal


Christopher Karenzi

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments