Amavubi stars wana kibarua mbele ya Sudan

Rwanda inachuana na Sudan katika ½ fainali ya Cecafa huku wenyeji Ethiopia wikipepetana na Uganda.

Timu mbili za Sudan na Rwanda zimefuzu kwa hatua ya nusu fainali ya michuano ya Cecafa baada ushindi katika michezo yao.

Sudani waliokua wakicheza na ndugu zao Sudan ya kusini walipata ushindi wa mabao 5-3 katika changamoto ya mikwaju ya penati baada ya kumaliza kwa sare ya 0-0 katika dakika 90 za mchezo.

Timu ya taifa ya Rwanda ikawaondoa mabingwa watetezi Kenya kwa changamoto ya mikwaju ya penati kwa mabao 5-3, baada ya kushindwa kupata mshindi katika dakika 90 .

Mchuano mwingine Nusu fainali ni kati ya Uganda na Ethiopia

Kikosi cha Ethiopia

Timu ya Taifa ya Uganda na Wenyeji Ethiopia zilikuwa timu za kwanza kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Cecafa 2015.

Wenyeji wa michuano hiyo Ethiopia wamesonga mbele kwa kuifunga timu ya Tanzania Kilimanjaro Stars kwa mikwaju ya Penati 4-3 baada ya suluhu ya 1-1 kwa dakika 90.
Nayo timu ya Uganda The Cranes iliichapa Malawi 2-0 kwa mabao ya Farouq Miya na Ceaser Okuti, nahivyo kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali.
Makuruki

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments