Ethiopia na Uganda zakata tikiti ya ½ fainali CECAFA

Michezo ya robo fainali ya michuano ya kombe la Cecafa Chalenji Cup imechezwa jumatatu hii mjini Adis Ababa, Ethiopia.

Timu ya taifa ya Uganda the cranes itakuwa imeizaba Malawi mabao 2-0 , huku timu ya Tanzania bara maarufu kama The Kilimanjaro stars ikichapwa na na Wenyeji Ethiopia kwa mikwaju ya penati baada ya kutoka sare ya bao 1-1.

Robo fainali ya pili itapigwa hapo jumanne Desemba mosi kwa Sudan kusini kukipiga na Sudan, Rwanda wakipepetana na Kenya.

Michezo ya nusu fainali itafanyika siku ya Alhamisi huku mchezo wa fainali na ule wa kumsaka mshindi wa tatu ikifanyika siku ya jumamaosi Desemba 5.

Christopher Karenzi

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments