Wanyarwanda kulinda usalama wa Papa Francis Centrafrika

Wanajeshi Rwanda walioko katika operesheni za kulinda amani nchini ya Jamhuri Centafrika ndio wanaoulinda usalama wa Papa Francis.

Kwa kawaida wanajeshi wa Rwanda ndio wanaolinda usalama wa rais Catherine Samba Panza wa Centrafrika.

Katika ziara yake barani Afrika, Papa Francis Jumapaili hili aliizuru Jamahuri ya Centrafrika.

Katika ikulu, Papa Francis aliwaomba wanainchi kuishi kwa amani, na kuacha ugomvi kati ya waisilamu na wakristo.
Picha zinazozunguka mitandaoni, zinaonyesha Papa Francis akilindwa na wanajeshi wa Rwanda walioko Centrafrika.

Centrafrika ilikumbwa na mashambulizi kati ya waisilamu na wakristo, takriban miaka mitatu imepita.

Mwanajeshi wa Rwanda (upande wa kushoto) mbele ya Papa Francis

Katika Misa, Papa Francis alishawishi wanainchi kutupa silaha ambazo ni wakala wa kifo, bali kujivika ukweli.

Inatarajiwa Jumatatu hii Papa Francis kuzuru msikiti mjini Bangui, kujadili na waumini wa dini la Islam.

Papa alitembelea Centrafrika baada ya Uganda na Kenya.

Ferdinand Maniraguha

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments