Papa amewasili Jamhuri ya Afrika ya Kati

Papa ameanza mkondo wake wa mwisho wa ziara yake katika mataifa ya Afrika

Papa Francis ameanza mkondo wake wa mwisho wa ziara yake katika mataifa ya Afrika Jumapili kwa kuwasili katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Bangui
Kiongozi huyo wa kanisa katoliki duniani aliwasili mjini Bangui muda mchache uliopita na kulakiwa kwa shangwe na nderemo na maelfu ya wakatoliki.

Aidha Papa Francis ametangaza nia yake kuu ni kuleta amani katika taifa hilo ambalo limekumbwa na mapigano ya kidini kati ya Waiislamu na Wakristo
Licha ya hofu ya usalama wake katika taifa hilo, Papa amesema ana moyo wa kutuma ujumbe wa amani na matumiani.

Image captionPapa francis alilakiwa na rais Catherine Samba katika uwanja wa ndege mjini Bangui

Kulingana na BBC Ziara ya papa Francis imewadia muda mfupi kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kuleta amani mwezi ujao.

Papa mara baada ya kuwasili nchini Afrika ya kati

Mbali na kuadhimisha misa katika mji mkuu wa Bangui, Papa anatarajiwa kukutana na viongozi wa Kiislamu na kutembelea msikiti mmoja mjini humo katika kitongoji kilichoathirika sana na mapigano cha PK5.
Papa Francis amekuwa katika ziara yake ya kwanza tangu atawazwe kuwa kiongozi wa wakatoliki duniani iliyoanzia Kenya Uganda na sasa inakamilikia Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Idadi ya watu : 4.6 million - 50% Wakristo, 15% Waislamu, 35% imani zingine
Imemkubwa na vita miaka na uongozi mbaya
Mapigano yameegemea imani na dini majuzi
Ilitawaliwa awali na mfalme Jean-Bedel Bokassa
Inautajiri mkubwa wa almasi
Inawalinda usalama wa umoja wa mataifa 10,000- tangu Septemba 2014
Ufaranza ndio iliyoitawala wakati wa Ukoloni
Ufaransa inawanajeshi 2000 huko tangu Decemba 2013

Makuruki

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments