Rwanda inahitaji ushindi ijumaa dhidi ya Somalia

Jacques Tuyisenge mfungaji wa magoli mawili katika mechi mbili akiwa pamoja na kocha

Timu ya taifa ya Rwanda Amavubi stars inahitaji ushindi dhidi ya Somalia ili ijihakikishie kusonga mbele kwa hatua ya ¼ fainali katika michuano ya Cecafa leo ijumaa tarehe 27 Novemba 2015.

Rwanda na Somalia zinachuana hivi punde saa sita na nusu majira ya Kigali

Rwanda, iliwashangaza wenyeji Ethiopia kwa kipigo cha bao 1-0 lililofungwa na mshambuliaji Jacques Tuyisenge katika mechi yafungua dimba, hadi kipenga cha mwisho kupulizwa vijana wa Rwanda waliondoka na alama 3.

Bao la kwanza la Rwanda katika dakika ya sita tayari limeishaingia mfungaji akiwa ni Habimana

Mechi ya pili Katika kundi la Rwanda, Kilimanjaro Stars imekuwa timu ya kwanza kukata tiketi ya kucheza robo fainali ya michuano ya Kombe la Chalenji baada ya kuifunga Rwanda 2-1,washambuliaji wakiwa ni Said Ndemla na Simon Msuva.

Ndemla alikuwa wa kwanza kutikisa nyavu za Rwanda (Amavubi) kwa mpira wa frii kiki iliyokwenda moja kwa moja kwenye nyavu za wapinzani wao katika dakika ya 18.
Kili Stars iliyoshinda mchezo wa kwanza kwa kuitandika Somalia mabao 4-0, iliandika bao la pili katika dakika ya 77 kupitia Msuva aliyeuwahi mpira ulishindwa kuchezwa na kipa wa Rwanda.

Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa, ulishuhudia kila upande ukifanya mashambulizi makali.

Stars inayofundishwa na Kocha Abadallah Kibadeni ilicheza vizuri na ilionekana kuimarika zaidi sehemu ya kiungo na ushambuliaji.

Wachezaji John Bocco, Himid Mao, Msuva na Elius Maguli wangeweza kufunga kama wangetumia vizuri nafasi walizopata kipindi cha kwanza.

Rwanda ilicheza vizuri zaidi robo ya mwisho ya mchezo ikifanya mashambulizi mara kwa mara kwenye lango la Kili Stars na kufanikiwa kupata bao hilo moja.

Kilimanjaro Stars sasa inasubiri kupambana na mwenyeji wa michuano hiyo, Ethiopia iliyofungwa bao 1-0 na kuwachapa Somalia 2-0 katika mechi ya pili.

Christopher Karenzi

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments