Tabia nchi : Papa aonya kuhusu kushindwa kwa mkutano wa kimataifa Paris

Papa Francis ameonya Alhamisi Novemba 26 mbele ya Umoja wa Mataifa mjini Nairobi kuhusu madhara ya "majanga" kama mkutano wa kimataifa kuhusu ongezeko la joto duniani unaoanza Jumapili mjini Paris, nchini Ufaransa, utashindwa.

"Nathubutu kusema, itakua janga. Kwa hiyo maslahi ya watu binafsi yawekwe kwenye manufaa ya wote katika mkutano huo", Papa Francis ameonya, akihutubia taasisi za Umoja wa Mataifa zinazoshughulikia masuala ya mazingira na malazi.

Mawaziri kutoka nchi sitini walikutana jijini Paris Jumapili Novemba 8 ili kuharakisha mazungumzo juu ya mkataba wa kimataifa ili kupiga vita ongezeko la joto duniani.

Rais wa Urusi Vladimir Putin atahudhuria mkutano wa kimataifa kuhusu ongezeko la joto duniani utakaofanyika Novemba 30.

Zaidi ya marais na viongozi wa serikali mia moja, ikiwa ni pamoja na marais wa Marekani na China watahudhuria mkutano huo.

RFI Kiswahili

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments