Rais Kagame aombwa kuruhusu marekebisho ya katiba


Waziri mkuu wa Rwanda Anastase Murekezi

Serikali ya Rwanda yaomba Rais wa jamhuri ya Rwanda Paul Kagame kuruhusu marekebisho ya katiba

Baraza la mawaziri liliketi jana jumatano kwenye village Urugwiro chini ya uenyekiti wake waziri mkuu Anastase Murekezi.

Baraza hilo limemuomba Rais wa jamhuri Kagame kuruhusu marekebisho ya katiba ya Rwanda ya tarehe 04 Juni 2003 na baadae kuomba ibadilishwe mwaka 2015.

Kikao cha baraza cha tarehe 25 Novenba 2015 kiliidhinisha mswada wa sheria wa mabadiliko kupitia Mswada huu wa sheria utakaofikishwa kwa rais baada ya

Wabunge na Maseneta wa Rwanda kuidhinisha mswada wa Katiba unaomruhusu Rais Paul Kagame kuwania muhula mwingine wa tatu katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2017.

Baraza la mawaziri limesisitiza kuharakisha mswada huu kwenye ibara yake ya 109 na 193 ya katiba ya taifa ya tarehe 04 Juni 2003 kama ilivyorekebishwa.

Baraza la Seneti limepitisha sawa na Baraza la wawakilishi Oktoba 29, Ibara mpya 101 na 172, pamoja na Ibara zingine 175 za Katiba ijayo, ikiwa ni pamoja na Ibara sitini zilizpfanyiwa marekebisho ikilinganishwa na toleo lililopitishwa na Baraza la Wawakilishi Oktoba 29 mwaka huu.

Ibara mpaya ya 101 inapunguza muhula wa rais Kutoka miaka saba hadi mitano na mihula inapaswa kuwa miwili tu. Lakini Ibara mpya ya 172 inasema kwamba marekebisho hayo yataanza kutekelezwa baada ya miaka saba ya uongozi kati ya mwaka 2017 na 2024, ambapo Rais wa sasa "aliye madarakani" bado ana haki ya kugombea, na kisha kwa mihula miwili ya miaka mitano kila mmoja iliyopangwa katika Ibara mpya ya 101.

Wanyarwanda milioni 3.7 nchini kote walitia saini kwenye barua inayoomba Rais Paul Kagame, mwenye umri wa miaka 58 kusalia mamlakani.

Rais wa sasa "aliye madarakani" bado ana haki ya kugombea, na kisha kwa mihula miwili ya miaka mitano kila mmoja iliyopangwa katika Ibara mpya ya 101.

Marekebisho haya ya Katiba yamewasilishwa na serikali kama matunda ya jitihada za raia, lakini waangalizi wengi wana mashaka na ukweli kuhusu madai hayo na kuona kama ni ujanja ulioandaliwa na viongozi wa Rwanda.

Christopher Karenzi

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments