"Hakuna askari wetu aliyeuwawa Sudani Kusini " Jeshi la Rwanda

Jeshi la Rwanda limetangaza kuwa hakuna askari wake alieuwawa Sudani Kusini.

Hii ni baada ya habari zilizotangazwa na gazeti la Bloomeberg kwamba mmjoa wa askari wa Rwanda alipigwa risasi na mwenzake tarehe 23 Novemba na kufa mara hiyo.

Rwanda ni miongini mwa nchi zinazokuwa na wanajeshi wake Sudani Kusiini katika ujumbe wa Umoja wa kimataifa wa kurudisha amani.

Msemaji wa Jeshi la Rwanda Brig Gen Joseph Nzabamwita amekanusha taarifa hiyo, na kuthibitisha kwamba askari wa Rwanda Sudan Kusini wote wazima.

Brig Gen Nzabamwita amefafanua kuwa aliyekufa ni askari wa nchi nyingine baada ya kufyatuliwa risasi na mwenzake pia ambaye si mnyarwanda, baada ya kujeruhiwa, askari huyo akapelekwa katika zahanati ya wanajeshi wa Rwanda mjini Juba.

Muda si mrefu alipoletwa zahanatini, askari huyo aliyekuwa amejeruhiwa alikufa.

Jeshi la Rwanda limesema limetuma ujumbe wa kutuliza moyo wafiwa.

Ferdinand Maniraguha

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments