Nsengimana Jean Bosco bingwa wa Tour du Rwanda 2015

Nsengimana Jean Bosco mchezaji wa timu ya Rwanda Kalisimbi atawazwa kuwa bingwa wa Tour du Rwanda 2015. Alivaa jezi ya njano tangu mwanzo kabisa wa mashindano hadi kufikia jumapili

Mashindano ya kimataifa ya kuendesha baiskeli Tour of Rwanda yaliyoanza tarehe 15 Novemba yalifikia kilele chake jumapili tarehe 22 novemba 2015

Mashindano haya yaliwaleta kwa pamoja wachezaji 69 kutoka mataifa mbali mbali duniani. waliomaliza mtihani huu wa kuzunguka Rwanda nchi ya milima elfu moja ni 47 pekee.

Mvua kubwa iliyonyesha mjini Kigali siku ya nane na ya mwisho, haikuzuia umati mkubwa wa mashabiki kshangilia waendesha baiskeli kutoka mataifa mbali mbali duniani na hata katika hafla ya kutunikia wahindi zawadi zao.

Nsengimana Jean Bosco mchezaji wa timu ya Rwanda Kalisimbi ametawazwa kuwa bingwa wa Tour du Rwanda 2015, akikimbia umbali wa km 928.4 akitumia muda wa saa 23h 54’ 50’’ kwa muda wa siku nane.

Alifuatwa na wanyarwanda wengine watatu ARERUYA Joseph TEAM RWANDAAKAGERA aliyetumia muda wa saa 23h 56’ 35’’ , HAKUZIMANA Camera TEAM wa timu ya RWANDA MUHABURA aliibuka na nafasi ya tatu akitumia muda wa saa 23h 57’ 35’’ 02’45’’

EYOB Metkel wa timu ya taifa ya ERITREA alinyakua nafasi ya nne akitumia muda wa saa 23h57’52’.

Mchezaji AMANUEL Meron anayeichezea timu BIKE AID ERI kutoka Ujerumani akiwa na Uraia wa Eritrea alitawazwa bingwa kwa kupanda milima meilleur grimpeur kwa lugha ya kifaransa alitumia muda wa saa 24h17’17’’ Bingwa wa mbio hizo Nsengimana kwa jumla alimzidi dakika 22’27’’

Sempoma Felix ni kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Rwanda , baada ya mashindano haya amesema kwamba ushindi huu umetokana na ufanisi bora wa maandalizi.

Naye Nsengimana Jean Bosco akiongea na waandishi wa habari amefurahia ushindi na hapa namnukuu.
Jambo la kwanza nashukuru mwenye mungu kupata ushindi huu, kazi haikuwa rahisi , nashukuru pia wenzangu tulioshirikiana bega kwa bega kutwaa ushindi huu, lengo letu limekamilika, tumekamilisha mashindano haya kwa amani hakika tumefurahi sana.
Aidha, Nsengimana Jean Bosco ametoa shukran za dhati kwa Rais wa Rwanda Paul Kagame aliyewapa baiskeli za thamani. Amesema kuwa si kila mtu kutoa zawadi kama hiyo.

Mashindano haya Tour Rwanda tangu yaanze mwaka 2009, yalitawaliwa na mmaroko Adil Jelloul, 2010 Daniel Teklehaimanot wa Eritrea , mwaka 2011 ilinyakuliwa na mmarekani Kiel Reijnen, mwaka 2012 ni Daren Lill kutoka Afrika ya kusini, 2013 alitawazwa Dylan kutoka Afrika ya Kusini, mwaka jana 2014 mnyarwanda

Ndayisenga Valens alishindwa kumaliza mashindano zikiwa zinasalia siku tatu kabla ya kukamilisha mashindano yenyewe kutokana na ugonjwa.

Hatimaye mwaka 2015 Nsengimana Jean Bosco ametawazwa bingwa na waziri wa Rwanda wa michezo na utamaduni Julienne Uwacu.

Christopher Karenzi

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments