Interpol kufuta wanyarwanda 40 kwenye hati ya mashitaka iliyotolewa na Hispania

Lt Gen Karenzi Karake, aliyekuwa kwenye orodha wanyarwanda wanaotafutiwa na Interpol

Tawi la polisi la kimataifa mjini Madrid Hispania limetoa tangazo likifuta hati ya mashitaka iliyotolewa kwa ombi la mahakama ya Hispania dhidhi ya makamanda wanyarwanda wapatao 40.

Interpol ilisambaza karatasi za kuwatia mbaroni wanyarwanda 40, baada ya kuombwa na Hispania ili wajitetee kuhusu shitaka lilokuwa linawakabiri la vifo vya watu kati ya mwaka 1995-1997 na vifo vya wahispania watatu waliokuwa Rwanda wakati huo.

Mwezi Juni mwaka huu mkuu wa ujasusi Lt Gen Karake Karenzi alikamatwa mjini London kwa hati hiyo lakini baadaye akaachiwa huru kwa kukosekana kwa ushahidi.

Octoba mwezi huu mahakama kuu ya Hispania yalifuta shitaka la wanyarwanda hao tena kwa kukosa ushahidi.

Interpol imesema kuwa ilichunguza wanyarwanda hao moja kwa moja, na kuona hawafai kuwindwa na Interpol ukilinganisha na wajibu wake.


Ferdinand Maniraguha

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments