Seneti ya Rwanda imepitisha rasimu ya Katiba

Jumanne hii tarehe 17 Novemba Seneti ya Rwanda imepeitisha rasimu ya katiba ya Rwanda inayorekebishwa kwa kura 26 za maseneti 26 waliohudhuria.

Rasimu hiyo ya katiba ina vipengele 177, ambapo kuna kipengele kinachomruhusu rais wa leo kugombea mihula mingine baada ya kumaliza mihula yake miwili anayoruhiswa na katiba ya leo.

Baada ya kupitisha rasimu ya katiba, rasimu itapelekewa wabunge, baada ya kuyipitisha ipelekewe waziri mkuu, ambapo itatoka ikielekezwa kwa rais wa Jamhuri.

Rais ndiye atakayetanagza tarehe ya kura ya maoni.

Mkuu wa seneti Bernard Makuza ameviambia vyombo vya habari kuwa lazima kura ya rais ifanyike, ingawa pia rais Kagame anayeonekana anapendwa na raia atagombea.

Ferdinand Maniraguha

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments