"Kagame hawezi kutupa ombi la wanyarwanda la kuwaongoza tena" Gen James Kabarebe

Gen James Kabarebe

Waziri wa ulinzi Gen James Kabarebe amesema rais Paul Kagame hawezi kutupa mbali ombi la wanyarwanda la kuendelea kuaongoza.

Tangu Mei mwaka huu mamilioni ya raia waliandikia bunge barua wakiomba rais Kagame aendelee kutawala baada ya mwaka wa 2017 ambapo atakapomaliza awamu zake mbili anazokubaliwa na katiba.

Raia walikuwa wakiomba katiba isiyomruhusu Kagame kuwania kipindi kingine irekebishwe.

Katiba hiyo sasa maandalizi ya kuirekebishwa yanaendelea bungeni, lakini rais Kagame hajatangaza ikiwa atawania awamu nyingine au la.

Hata hivyo, Waziri Gen Kabarebe akihutubia wananchi jumapili hii wakati wa kufunga rasmi mwezi wa uzalendo mjini Kigali, alisema kwamba rais Kagame hawezi kukana ombi hilo.

"Sijazungumza naye lakini nadhani hawezi kukana. Huenda akiombwa na wazungu au viongozi kama sisi anaweza kukana, lakini akiombwa na raia , hawezi. Nchini hakuna kinachozidisha uwezo wananchi." Alisema Jenerali Kabarebe

Waziri Kabarebe amewakumbusha waliokusanyika kwenye uwanja wa Kicukiro kwamba Kagame hana nyota ya uongozi.

Kwake Kabarebe, Kagame alikataa kuongozi baada ya vita vya ukombozi mwaka 1994, akisema kuwa hataki madaraka.

"Mheshimiwa Kagame hakugombania madaraka...tulipomaliza kukomesha mauaji ya kimbari mjini Kigali, tulikutana naye sehemu za Kanombe tukamuambia eti serikali ya wauaji inatoweka, sasa wewe rais." Alisimulia Kabarebe

Na kuongeza : "Sisi tuliomuomba, tulikuwa maafisa wakuu jeshini.Alituangalia na kutujibu, mimi sikugombania kuwa rias, sitaki.Tuliondoka na hasira."

Katika katiba inayorekebishwa bungeni kuna kipengele kimachomruhusu rais aliye madarakani wakati wa kurekebisha katiba, kuwa anaweza kuwania awamu nyingine ya miaka saba , na kugombea nyingine mbili moja ikiwundwa na miaka tano.

Ferdinand Maniraguha

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments