“Rwanda tuko tayari kupokea michuano ya CHAN” Rais Kagame

Rais wa Rwanda ameahidi kuwa Rwanda itapokea ipasavyo michuano ya kombe la Afrika kwa timu za mataifa zenye wachezaji wa ligi ya nyumbani (CHAN).

Rais Kagame alitangaza hivi katika sherehe za kufanya dro za michuano hiyo Jumapili tarehe 15 Novemba mjini Kigali.

CHAN 2016 itaanza tarehe 16 Januari hadi 7 Februari.
Kagame amesema ni heshima kubwa Rwanda kupokea michuano kama hiyo ya cheo cha juu barani na kuwataka mashabiki wamiminike uwanjani wingi kushabiki timu zao.

Rais Kagame ameomba pia wachezaji kuonyesha mashabiki mchezo wa kibingwa, ili wasikate tamaa.

Kagame ameendelea kuhakikisha kwamba Rwanda itafanya liwezekanalo ili michuano hiyo iende vizuri.

Rais makamu wa shirikisho la soka barani Afrika Almamy Kabele amesema hana budi Rwanda itapokea vizuri CHAN.

Timu ya taifa ya Rwanda Amavubi aimejikuta katika kundi la mabingwa wa soka barani Afrika. Kundi hilo linajengwa na Rwanda, Maroc, Cote d’Ivoire na Gabon.

Kundi la pili : DRC, Ethiopia, Cameroun, Angola

Kundi la tatu : Tunisia,Guinea, Niger, Nigeria
Kundi la nne : Zimbambwe, Zambia, Uganda, Mali

Makuruki

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments