Waendesha baiskeli wakubali kurudi katika kambi ya mazoezi

Waendesha baiskeli wa Team Rwanda wamerudi katika kambi ya mazoezi wilayani Musanze baada ya kutaka kususia mashindano ya Tour du Rwanda.

Waendesha baiskeli hao walikuwa wakiomba dola 3000 za marekani walizokuwa wameahidiwa baada ya kushinda mashindano ya Tour du Rwanda mwaka uliopita.

Baadhi yao waliokuwa wanaomba fedha hizo walifukuzwa kambini kwa kutuhumiwa upotevu wa nidhamu.

Viongozi wa chama cha mbio za baiskeli wamesema kwamba wamezungumza na waendesha baiskeli na kutatua matatizo yote yaliyoko, halafu wakaamuwa kurudi kambini.

Miongoni mwa waendeshaji baiskeli hao ni Hadi Janvier nahodha wa timu ya taifa,Valens Ndayisenga bingwa mtetezi wa mbio hizo na bingwa mara nne wa ’Tour of Rwanda’ Abraham Ruhumuriza.

Rwanda ilinyakuwa nafasi ya kwanza katika mashindano ya Tour du Rwanda mwaka jana.

Mashindano hayo anatarajiwa kufanyika kutoka tarehe 15 Novemba 2015.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments