Kiswahili kinaweza kuwa lugha rasmi nchini Rwanda

Baraza la maseneti

Seneti ya Rwanda inatangaza kuwa Kiswahili kibaweza kuongezwa katika lugha rasmi zinazokubaliwa katika katiba ya taifa.

Rasimu ya katiba ambayo inaandaliwa , kipengele chake cha 8 kinabaini kuwa lugha rasmi ni Kinyarwanda, Kiingereza na Kifaransa, lakini na kuacha nafasi kwa lugha nyingine ambazo zimeonekana ni muhimu kwa taifa.

Jumatatu hii tarehe 9 Novemba maseneti wanaokuwa katika tume ya siasa na ustawi wa jamii walipojadili kuhusu katiba kipengele kwa kipengele, wamesema kuwa kuna uwezekano wa Kiswahili kuwa miongoni mwa lugha rasmi kutokana na Rwanda kuwa mshiriki wa Jumuiya ya Afrika ya mashariki.

Hon Uwimanimpaye, mbunge ambaye ni mmoja wa walioandaa rasimu ya katiba amesema kwamba walitafakali kuhusu Kiswahili kuwa lugha rasmi.

Amenukuliwa : "Tulipozungumza kuhusu kipengele hiki, tulifikili kuhusu Kiswahili, tukisema kwamba wakati itakapokuwa lazima kukitumia, kitawekwa kwenye orodha."

Maseneti wameendelea kufafanua kwamba si Kiswahili pekee ambacho kina ruhusa ya kuingia katika lugha rasmi, bali na lugha nyingine serikali itakapoiona ni muhimu.

Katiba ya kale ilikuwa hairuhusu lugha nyingine kuwa rasmi isipokuwa Kiingereza, Kinyarwanda na Kifaransa.

Maniraguha Ferdinand

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments