Rwanda kutengeneza kompyuta zake kwa mara ya kwanza

Kompyuta ya kwanza iliyotengenezewa Rwanda itafika sokoni jumatatu tarehe 9 Novemba mwaka 2015.

Kompyuta hizo z itakuwa na alama ya kiwanda cha Positivo-BGH na kwa msaada wa kampuni Africa Smart Investment Distributor kompyuta hizo zitaenezwa pande mbalimbali duniani.

Viongozi hawakutangaza bei ya kompyuta moja, lakini wamesema itaulizwa kwa bei nafuu ukilinganisha na kompyuta zinazotoka ng’ambo.

Kwa kawaida kompyuta nchini Rwanda ilikuwa inauzwa kwa elfu mia mbili kwa ujumla.Kwa mara ya kwanza kompyuta elfu 150 zitawekwa sokoni.

Kiwanda kinachotengeneza kompyuta hizo kina uwezo wa kutengeneza kompyuta elfu 60 katika mwezi mmoja.

Utengenezaji wa kompyuta hizo ulikamilika kukitumiwa bilioni nne dola za Marekani.

Ferdinand Maniraguha

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments