Rais Kagame kuhudhuria kuapishwa kwa DK Magufuli wa Tanzania

1

Rais wa Jamhuri ya Rwanda Paul Kagame ni miongoni mwa marais watakaohudhuria sherehe za kumuapisha rais mpya wa Tanzania DK John Joseph Pombe Magufuli, kama inavyotangazwa na Wizara ya mambo ya nje ya Tanzania.

Sherehe za kumuapisha DK Magufuli zitafanyika Alhamisi tarehe 5 Novemba kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar Es Salaam.

Marais watakaoshuhudia ni pamoja na Robert Mugabe wa Zimbabwe, Yoweri Museveni (Uganda), Paul Kagame (Rwanda) Uhuru Kenyatta (Kenya), Joseph Kabila (DRC), Jacob Zuma (Afrika Kusini) Filipe Nyusi (Msumbiji) na Edgar Lungu (Zambia).

Tanzania na Rwanda ni miongoni mwa nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika ya mashariki.

Nchi hizi mbili mahusiano yao yaliharibika mwaka 2013, wakati rais Jakaya Kikwete aliposema kwamba ni vizuri Rwanda kuingia katika mazungumzo na waasi wa FDLR wanaotuhumiwa na serikali ya Rwanda kujitosa katika mauaji ya kimbari dhidhi ya Watutsi mwaka 1994.

Leo nchi hizo mbili zinatangaza kuwa uhusiano wao ni shwari na kuwa wataendelea kufanya liwezekanalo ili iendelee hivyo hivo.

Ferdinand Maniraguha

Changia hii habari na wenzako.

Comments 1

Tumia Comments