Vatican yawakamata wawili kwa kuvujisha siri

Makao makuu ya Papa Vatican imesema watu wawili imewakamata watu wawili mmoja akiwa kasisi wa kanisa hilo na mwingine mfanyakazi wa zamani wa makao ya papa kwa tuhuma kuvujisha nyaraka siri za kanisa hilo.

Wawili hao walikuwa wajumbe wa tume iliyoundwa na Papa Francis kwa ajili ya jukumu kuleta mabadiliko katika mfumo wa kifedha wa kanisa katoliki.

Uongozi wa juu wa kanisa hilo unaamini kwamba wawili hao walivujisha nyaraka muhimu za majadiliano ya tume hiyo kwa waandishi habari wanaofanya uchunguzi wa masuala ya rushwa ndani ya Vatican.

Nyaraka hizo ndizo zitakazotumika kuchapisha vitabu viwili vinavyotarajiwa kutolewa kuhusiana na utata wa hali ya kifedha wa Vatican.mmoja wa waandishi habari Gianluigi Nuzzi ambaye alichapisha moja ya nyaraka hizo mnamo mwaka 2012 ambaye anadai kupewa nyaraka hizo na mtangulizi wa Papa Francis .

BBC Kiswahili

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments