NEC imetangaza rasmi ratiba ya uchaguzi nchini Rwanda

Prof -Kalisa Mbanda, mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya taifa

Tume ya uchaguzi nchini Rwanda imetengaza rasmi ratiba ya uchaguzi itakayofuatiliwa katika miaka mitatu inayokuja.

Rwanda yajiandaa uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa, uchaguzin wa rais pamoja na uchaguzi wa wabunge na maseneti.

Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi nchini Rwanda Prof Kalisa Mbanda akitanagza rasmi ratiba hiyo amesema kwamba uchaguzi utakaofanywa kwanza ni wa viongozi wa serikali za mitaa.

Prof Mbanda ameongeza kuwa wagombea wataanza kujiandikisha mapema mwezi Novemba 2015, na upigaji kura utafanyika Mechi 2016.

Mpangilio wa uchaguzi unaonyesha kuwa uchaguzi wa rais utafanyika mwaka wa 2017, utafuatiliwa na wabunge mwaka 2015, mwishoni maseneti watakaochaguliwa mwaka 2019.

Prof Mbanda amehakikisha kwamba uchaguzi umeendelea kuwa shwari nchini Rwanda, na kuongeza kwamba itaendeela kuwa hivyo hivo kwa ushirikiano wa kila mtu.

Maniraguha Ferdinand

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments