Shambulizi laua 15 mjini Mogadishu

Somalia inasema kuwa takriban watu 15 wameuwa

Utawala nchini Somalia unasema kuwa takriban watu 15 wameuawa wakati wanamgambo waliposhambulia hoteli moja mjini Mogadishu.

Hoteli hiyo ambayo iko kwenye moja ya mitaa yenye shughuli nyingi mjini humo mara nyingi hutumiwa na wabunge na maafisa wa serikali.

Kundi la kiislamu la al Shabaab lilisema kuwa lilitekeleza shambulizi hilo.
Vikosi vya muungano wa Afrika vinasema kuwa vimechukua udhibiti wa hoteli hiyo baada ya mapigano makali.

Ripoti zinasema kuwa mlipuko huo ulifuatiwa na ufyatulianaji mkubwa wa risasi.

BBC

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments