Rais Kagame anaweza kuongoza miaka mingine 17

Bunge la Rwanda limepiga kura kuidhinisha mabadiliko ya katiba, ambayo yatamwezesha rais Paul Kagame kugombea muhula wa tatu mwaka 2017, na kuweka uwezekano wa kubakia madarakani hadi mwaka 2034.

Kipengele cha 172 cha katiba kinasema kwamba kiongozi yeyote atakayeongoza baada ya mwaka 2017 atapewa miaka saba, ikimanisha kwamba Rais Kagame au mtu mwingine atakayeshinda uchaguzi, ataongoza miaka saba wakati miaka mitano izayozungumzwa katika kipengele cha 101 cha mswada wa sheria katika katiba kitaanza baada ya mwaka 2024.

Katika mabadiliko hayo ya katiba, wabunge walipunguza urefu wa muhula kutoka miaka saba hadi mitano, lakini kwa namna ya kipekee Rais Kagame ameruhusiwa kugombea kwa miaka mingine saba kwa mhula ujao, na baada ya hapo anaweza kugombea kwa mara ya mwisho muhula wa miaka mitano.

Spika wa bunge Bi Mukabarisa Donatille alipoulizwa ikiwa kipengele kinachoambatana na miaka saba ikiwa rais wa jamhuri Kagame Paul akikataa kugombea kiti cha urais, amesema kwamba sheria haimruhusu rais Kagame peke yake kwani hata yeye binafsi hajaamua ikiwa atagombea kwenye uchaguzi ujao.

Mabadiliko hayo yametokana na maombi ya umma, huku wapinzani chama cha Green Party wakishikilia msimamo wao wa kupinga mswada wa sheria wa katiba kutoubadili.

Kwa jumla wabunge waliopitisha mswada wa sheria wa katiba yote ni vipengele
177, Uamuzi huo wa bunge utahitaji ridhaa ya seneti, kabla ya kupigiwa kura ya maoni na wananchi.

Rais Kagame amechaguliwa kuwa rais mara mbili, mwaka 2003 na mwaka 2010.

Christopher Karenzi

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments