Rwanda : Awamu moja ya rais ni miaka mitano badala ya saba

Bunge la Rwanda limeidhinisha mabadiliko ya katiba yanayopendekeza kuwa Rais Kagame anaweza kuchaguliwa kwa awamu nyingine moja na kupunguza miaka ya awamu kutoka miaka 7 na kupunguzwa miaka mitano.

Jumatano wiki hii, ndipo wabunge waliketi na kuidhinisha baadhi ya vipengele vya katiba. Wabunge wameidhinisha mswaada kuwa awamu moja ya rais ni kutoka miaka saba hadi miaka mitano pia waliidhinisha kuwa Rais Kagame anaweza kuchaguliwa kwa awamu nyingine moja ikiwa ni ya tatu.

Mapendekezo mengine yaliyoidhinishwa na wanyarwanda wengi, wanadai kuwa baada ya kuijenga upya uchumi wa taifa hilo uliosambaratika baada ya mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi mwaka wa 1994, hakuna sababu ya kumuondoa Rais Kagame madarakani.

Wananchi wengi waliopeleka barua zao kwenye Baraza la bunge, walipendekeza kipengele cha 101kibadilishwe.

Wabunge mbali mbali wameomba maelezo kuhusiana na kupunguzwa kwa awamu za rais wa jamhuri kutoka miaka saba na kushushwa hadi miaka mitano wakati maelezo tosha yalikuwa yametolewa na kueleweka.

Makamu mwenyekiti wa bunge la taifa Bi Uwimanimpaye Jeanne d’Arc, alifafanua kuwa awamu moja ya miaka mitano iliyoidhinishwa, ilitokana na mapendekezo pamoja na maoni ya wananchi wenyewe, kadhalika katika mataifa ya jumuiya ya Afrika ya mashariki awamu ya rais wa jamhuri haizidi miaka mitano.

Kati ya wabunge 75 waliohudhuria katika kikao cha baraza , 72 waliidhinisha mmoja akachagua hapana , mwingine hakuchagua , moja ikaharabika.

Christopher Karenzi

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments