Profesa Jay ashinda kiti cha ubunge TZ


Msanii wa Bongo Joseph Haule maarufu kwa jina ’Profesa Jay’ ndiye msanii wa hivi karibuni kuwahi kushinda kiti cha ubunge nchini Tanzania.

Msanii huyo wa muziki wa Rap alitangazwa mshindi wa kiti cha eneo bunge la Mikumi katika uchaguzi huo baada ya kupata kura 32,259.

Profesa Jay ambaye alikuwa akiwania kiti hicho kwa tiketi ya chama cha CHADEMA alimshinda mpinzani wake wa Chama cha mapinduzi CCM, Jonas Nkya ambaye alijipatika kura 30,425.

Msanii huyo ni wa pili sasa kuchaguliwa baada ya meneja wa bendi ya Yamoto Said Fella kuchaguliwa kama diwani wa wadi ya Kilungule jimbo la Mbagala

BBC

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments