Rwanda yapokea mkutano unaojadili demokrasia barani Afrika

Mananchi anatakiwa kupewa nafasi katika Nyanja ya demokrasia
Balozi Fatuma Ndangiza

Kuanzia jumatano wiki hii tarehe 28 Oktoba 2015 mjini Kigali kunafanyika mkutano unaojadili demokrasia na uongozi bora katika mataifa barani Afrika.

Mkutano huo unakuja wakati mataifa mengi ya ukanda huu yakiwa kwenye mchakato wa uchaguzi ambapo mwananchi anatakiwa apewe neno, hata hivyo utakuta wananchi wakati kama huu wa uchaguzi wanabugudhiwa kutokana na kutoa fikra zao.

Yapata zaidi ya miaka 50 mataifa ya Afrika yakiwa yametoka kwenye ukoloni lakini bara hili limekuwa likirudi nyuma kimaendeleo ukilinganisha na mabara mengine ikiwa ni pamoja na siasa, uchumi na mengine...

Jumatano tarehe 28 Octoba, Rwanda itapokea mkutano unazungumzia demokrasia na uongoi bora barani Afrika, mkutano huo utajadli masuala mbali mbali ya bara hili katika nyanja tofauti zikiwemo siasa, uchumi, usalama na mengine..

Balozi Fatuma Ndangiza kiongozi msaidizi wa taasisi ya taifa ya uongozi bora RGB, akiongea na waandishi wa habari amesema kwamba wananchi wa Afrika wanahitaji kufafanuliwa kujua haki zao.

Christopher Karenzi

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments