Aliyekuwa waziri wa serikali katika wizara ya elimu aachishwa kazi

Nsengiyumva Albert wakati alipokula kiapo kuanza rasmi shughuli za ujenzi wa taifa ( Februari 2013)

Aliyekuwa waziri wa serikali katika wizara ya elimu akihusika na shule za ufundi (TVET) NSENGIYUMVA Albert, ameachishwa kazi baada ya miaka miwili akiwa kwenye wadhfa huo.

Kwa mujibu wa tangazo lililosainiwa na waziri mkuu, linaeleza kwamba kiongozi huyu Nsengiyumva Albert, amesimamishwa kazi na rais wa jamhuri Paul Kagame ikizangatiwa uwezo anaopewa na katiba ya jamhuri ya Rwanda , hususan katika kipengele chake cha 116..

Nsengiyumva Albert alipewa wadhfa wa waziri wa serikali katika wizara ya elimu akihusika na shule za ufundi (TVET) kuanzia mwezi februari 2013

Karenzi Christopher

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments