UCHAGUZI 2015 : YANAYOJRI TANZANIA

MATUKIO MBALI MBALI YA UCHAGUZI NCHINI TANZANIA YAKIWEMO MATOKEO YA UCHAGUZI

Waangalizi wa uchaguzi

Mkuu wa waangalizi wa muungano wa Ulaya katika uchaguzi mkuu wa Tanzania Judith Sargentini, amesema ukosefu wa jitihada pamoja na uwazi ndio sababu ya tume za uchaguzi za NEC na ZEC kukosa imani za vyama vyote vya kisiasa.

Amesema kwamba licha ya maandalizi mazuri kutoka tume hizo za uchaguzi, kutokuwepo kwa uwazi na ukosefu wa habari muhimu kuhusu sajili ya kupiga kura pamoja na mipaka katika majimbo mbali na mbinu inayotumiwa kutangaza matokeo ndio sababu zilizoathiri imani ya vyama hivyo kwa tume hizo za uchaguzi.

Chama cha Upinzani kisiwani Zanzibar CUF kimetoa taarifa kikisema kinasikitishwa na mda unaochukuliwa na tume ya uchaguzi kisiwani humo kutoa matokeo.Kimesema kuwa hakioni sababu ya tume hiyo kutoa matokeo nusu nusu licha ya kuwa matokeo ya majimbo yote 54 yamehesabiwa kujumlishwa na kutolewa.

kutangazwa Zanzibar

Tume ya uchaguzi kisiwani Zanzibar imesitisha utangazaji wa matokeo kwa muda baada ya umeme kukatika. Hata hivyo imeahidi kuendelea na matokeo hayo baada ya umeme kurudi muda mfupi baadaye.

Biashara zimeanza kufunguliwa mjini Dar es Salaam nchini Tanzania huku wengi wa wa wafanyibiashara wakiendelea kufunga biashara zao. Hata hivyo, baadhi ya wafanyabiashara wanasema kuwa wataendelea kuzifunga hadi rais mpya atakapotangazwa.

Mawaziri watano wa serikali inayomaliza muda wake wameanguka kwenye uchaguzi katika majimbo yao,huku wagombea wengine wa Ubunge maarufu nao wakiangushwa na Kamba ya upinzani katika matokeo ya kura yanayoendelea kutolewa kufuatia uchaguzi mkuu nchini humo uliofanyika Jumapili.

Mawaziri hao watano wa serikali ya Jakaya Mrisho Kikwete inayomaliza muda wake ni Stephen Wassira Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Dk Steven Kebwe Naibu Waziri wa Afya, Christopher Chiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayehusika na Uwekezaji na Uwezeshaji, Anne Kilango Malecela Naibu Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi na Omar Nundu aliyewahi kuwa Waziri wa Uchukuzi.

Mawaziri hao walioangushwa katika majimbo yao wanaungana na wabunge wengine maarufu katika Bunge la Kumi la Tanzania waliong’ara ambao kwa sasa wameshindwa kurejea.

Hata hivyo pia wamo mawaziri wa Zamani Cyril Chami na Omary Nundu. Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania inaendelea kutangaza matokeo ya Ubunge na Urais.

Tayari tume ya uchaguzi imetoa matokeo ya majimbo 24 na bado inaendelea kutoa mengine zaidi.

Huko Zanzibar, visiwa ambavyo kando na kutawaliwa na Rais wa Jamhuri, huwa pia na rais wake, Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kufikia sasa imetangaza matokeo ya majimbo 13 kati ya majimbo 54 yaliyoko visiwani humo.

BBC

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments