Watani wa soka Rayon Sports na APR watoka sare

Michuano ya ligi kuu ya soka Azam Rwanda premier League iliendelea mwishoni mwa ligi, timu nyingi ziligawana alama

Jumapili

AS Kigali 0-0 Kiyovu Sports
Gicumbi FC 1-1 Mukura VS
Etincelles FC 1-0 AS Muhanga

Jumamosi

Rayon Sports FC 0-0 APR FC
Marines FC 0-0 Espoir FC
Sunrise FC 1-1 Police FC

Ujumaa

Rwamagana City FC 2-0 Bugesera FC
Musanze FC 1-2 Amagaju FC

Msimamo wa ligi kuu ya soka, timu ya AS Kigali inaendelea kuongoza kwa muda katika ligi kuu ya soka nchini Rwanda ikiwa inaongoza kwa alama 12 ikiwa sambamba na Police FC zikiwa na tofauti ya magoli huku APR FC ikija kwenye nafasi ya tatu.
Gicumbi FC ilishindwa kuwika nyumbani na kutoka sare ya kufungana na Mukura VS 1-1.

Gicumbi FC ndiyo ilifungua lango kupitia mlinzi wao Rucogoza Aimable maarufu Mambo, bila kupoteza muda Amani Mugisho Mukeshe wa Mukura, alisawazisha bao hilo.

Mechi ya kusisimua ilikuwa kati ya APR FC iliyokaribishwa na APR FC katika uwanja wa Amahoro- Remera, mjini Kigali Rayon ilitawala uwanja kwa asilimia kubwa lakini ikashindwa kufunga mechi vijana wa APR walikuwa pia na mipira ya kushtukiza na pasi za haraka haraka lakini kuliona lango ikashindikana.

Hadi kipenga kupulizwa timu zote zilikwenda sare ya kutofungana.
Makuruki

Wafungaji bora

1. Songa Isaie (Police Fc) 5
2. Murengezi Rodriguez (AS Kigali) 4
3. Kasirye Davis (Rayon Sports) 4
4. Peter Otema (Musanze FC) 4
5. Christopher Ndayishimiye (Mukura VS) 3
6. Rashid Mutebi (Gicumbi Fc) 3
7. Sugira Ernest (AS Kigali) 2
8. Saiba Claude Mumbere (Amagaju Fc) 2
9. Patrick Munyankindi (Sunrise Fc) 2
10. Andre Lomami (SC Kiyovu) 2

Makuruki

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments