Matokeo ya kura Tanzania kuanza kutangazwa Jumatatu

Kura zinahesabiwa katika uchaguzi mkuu wa Tanzania, ambapo wapigaji kura walijitokeza kwa wingi, kufuatana na taarifa ya Tume ya Uchaguzi.

Vituo vya kupigia vilifungwa jioni isipokuwa kwa wale ambao walikuwa vituoni, na bado hawakupiga kura.

Mashindano yamekuwa makali kati ya wagombea wa chama tawala cha CCM, na umoja wa vyama vya upinzani.
Mgombea wa chama tawala, John Magufuli, alipambana na waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ambaye ali

Polisi wamewasifu watu kwa kupiga kura kwa salama, maneno ambayo pia yalikaririwa na Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi, Ramadhan Kailima hapo awali.

Na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, amesema matokeo ya uchaguzi wa rais yatatoka baada ya siku nne.

BBC

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments