Tanzania inaweza kujifunza nini kutoka kwa Kenya ?

Baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007, Kenya ilishuhudia machafuko. Tanzania inaweza kujifunza kutokana na makosa ya nchi hiyo jirani ili kuhakikisha amani inatawala, wanasema wachambuzi.

Wakati hali ikionekana kuwa shwari kuelekea uchaguzi mkuu tarehe 25 Oktoba, kuna wasiwasi pia unaojitokeza wa kutokuwepo hali nzuri ya usalama nchini Tanzania wakati wa mchakato wa kupia kura na pengine hata baadaye.

Wasiwasi huo unatokana na sababu mbali mbali zinazotajwa na wadadisi wa mambo wanaofuatilia uchaguzi huo.

Mwaka 2007 Kenya ilitumbukia katika ghasia kubwa zilizosababisha umwagikaji mkubwa wa damu ambao hauwezi kusahaulika katika historia ya taifa hilo la Afrika Mashariki. Je, matukio ya Kenya yametoa somo gani kwa wananchi wa Tanzania wanaosubiri kupiga kura ?

Baada ya zoezi la kupiga kura mwananchi atatakiwa kwenda nyumbani au kuwa mita 200 ya eneo alikopigia kura.

Makuruki

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments