Marekani na Ulaya kuingilia mzozo wa Congo.

Raia wa Congo akiandamana kupinga uamuzi wa rais N’Guesso wa kujiongeza muda wa kuhudumu.

Makundi ya upinzani na ya kiraia kutoka Jamhuri ya Congo yamekutana Alhamisi na wawakilishi kutoka Marekani na Ulaya ili kuzungumzia kuhusu hali ya kisiasa nchini humo, ambapo kura ya maoni inayokusudia kumruhusu rais kuwania muhula wa tatu madarakani imezusha ghasia za kisiasa.

Perfect Kolelas, kiongozi wa chama cha upinzani cha Congolese Movement for Democracy and Integral Development, amesema ajenda zinajumuisha mashauriano ya kusaidia kumaliza ghasia za kisiasa nchini humo ambazo zimesababisha vifo vya watu wanne siku ya Jumanne.

Kolelas ameiomba jumuiya ya kimataifa ikiwemo Umoja wa Afrika kuingilia kati ili kuhakikisha katiba haikiukwi

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments