Wanajeshi wakomboa mateka 70 kutoka kwa IS


Wanajeshi wa Kikurdi wamekuwa wakijaribu kuwafurusha wapiganaji wa Islamic State maeneo ya Wakurdi

Wanajeshi wa Marekani wakishirikiana na wanajeshi wa Iraq wamefanikiwa kuwakomboa mateka 70 waliokuwa wakizuiliwa na wapiganaji wa Islamic State (IS) nchini Iraq.

Idara ya ulinzi ya Marekani imesema operesheni ya kuwakomboa mateka hao ilitekelezwa baada ya kubainika kwamba walikuwa karibu kuuawa.
Lakini mwanajeshi wa Marekani aliyejeruhiwa kwenye operesheni hiyo amefariki.
Ndiye mwanajeshi wa kwanza kufariki tangu kuanza kwa operesheni ya wanajeshi wa Marekani dhidi ya IS mwaka jana.

Kwenye operesheni hiyo iliyotekelezwa mapema Alhamisi karibu na mji wa Hawija kaskazini mwa Iraq, wapiganaji wa IS walinaswa na wengine kadha kuuawa, Pentagon imesema.

Jumla ya mateka 70 walikombolewa, maafisa wa ulinzi wamesema, wakiwemo Waarabu wa dhehebu la Wasunni, wanajeshi 20 wa Iraq na wanachama wa IS waliokuwa wakizuiliwa baada ya kushukiwa kuwa majasusi.

Hakuna watu wowote wa asili ya Kikurdi waliokombolewa, maafisa wa Pentagon na Wakurdi wamesema.

Habari za awali zilikuwa zimedokeza kwamba huenda kulikuwa na Wakurdi waliookolewa.

Wanajeshi wa Marekani walishiriki kwenye operesheni hiyo baada ya kupokea ombi kutoka kwa serikali ya jimbo lenye Wakurdi wengi Kirkuk.

Makuruki

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments