Rwanda yachaguliwa kuingia katika kikao cha uchumi kwenye umoja wa mataifa UN

Rwanda na mataifa mengine 18 duniani yamechaguliwa kuingia katika kikao cha uchumi na ustawi wa jamii katika umoja wa mataifa.

Kikao hicho kiliidhinishwa kwa alama 182 kati ya 187 ambapo nchi zilizochaguliwa ni pamoja na Rwanda, Afghanistan, Algeria, Australia, Chile, Jamhuri ya Czech, Guyana, Iraq, Italia, Libani, Nigeria, Peru, Moldova, Somalia, Afurika ya Kusini, Vietnam na Umarekani.

Kuchaguliwa kwa Rwanda ni hatua nyingine iliyopigwa inayoonyesha mipango thabiti ya maendeleo katika Umoja wa mataifa.

Rais wa Rwanda Paul Kagame aliteuliwa kuwa kiongozi wa baraza tendaji linalohusu shughuli za maendeleo ya kudumu, SDGs.

Mwakilishi wa Rwanda kwenye umoja wa mataifa Bal.Eugene Gasana

Hatua hii imekuja baada ya Rwanda kuwa miongoni mwa mataifa yaliyotoa mfano bora kufikia malengo ya milenia, MDGS, itakayofikia kilele chake mwaka huu.

Rwanda itaanza majukumu ya kuwa katika baraza la UN tarehe mosi januari 2015 ambapo itakuwa na muda wa miaka mitatu ndani ya baraza hilo.

Aidha taifa hili lililoko katika Afrika ya mashariki, lilianza kuwa mwanachama wa Umoja wa mataifa tarehe 18 Septemba 1962, iliingia kwenye baraza la usalama kwenye UN kati ya mwaka 1994 na 1995.

Kati ya mwezi Aprili na Mata Julai 1994, iliwakilishwa na serikali iliyokuwa inafanya mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi.

Rwanda ilirudi tena mwaka 2013 na 2014, iliongoza baraza la usalama tawi la Umoja wa mataifa.

Christopher Karenzi

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments