Kocha wa Rayon Donadei asimamishwa mechi moja dhidi ya APR FC


Mkufunzi wa Rayon David Donadei amekataliwa kuinoa timu hiyo wakati watakapochuana na APR FC

Mkufunzi wa soka wa club ya Rayon Sports, David Donadei, amesimamishwa kuinoa timu hiyo ambayo ina kibarua na APR FC mwishoni mwa wiki hii tarehe 24 octoba 2015.

Ni mchezo wa ligi kuu ya soka daraja la kwanza utakaofanyika katika uwanja wa taifa wa Amahoro Remera.

Katibu mkuu na msemaji wa Rayon Sports, Gakwaya Olivier, amekili kuwa wamesimamisha mechi moja kuinoa wakati watakapochuana na APR , baadae ataendelea na shughuli zake.

Akiongea na Redio 10, mkufunzi David Donadei ametoa matamshi makali dhidi ya timu yake Amesema : ‘’Kamati ya Rayon ni wezi, pia ni wadanganyifu.

Wakati huu niko hotelini Nyanza, Nyanza Heritage. Hawajalipa hoteli, yapata sasa mwezi na nusu tangu nifike hapa, manager yuko pembeni yangu".
"Jumamosi nilirudi baada ya mechi nikiwa pamoja na wachezaji, Hoteli iliniweka nje ya mlango kwani kamati ilikuwa haijalipa.

Manager aliniambia kuwa hawezi kunipa chumba wakati kamti haijamlipa’’.
David alipokuwa nchini ufaransa hivi majuzi , alielezea wachezaji kuwa amejiuzulu kuinoa timu ya Rayon, baadhi ya vyombo vya habari vilianza papo hapo kutangaza habari hiyo.

Kocha huyo alirudi nchini mwake Ufaransa, kuchukua vifaa vyake, akiwa huko alituma ujumbe mfupi kwa njia ya sms akiwaambia wachezaji kuhusu uamuzi huo ambao hata hivo ulikanushwa na msemaji wa Rayon sport Gakwaya.

Katibu mkuu wa Rayon Sports , amebaini kuwa kocha huyo anafanya mahojiano na vyombo vya habari akiviambia habari tofauti tofauti kuhusu matatizo yanayoikumba timu yao , hiyo inaashiria kutotoa uzito wa mechi kubwa kati yao na APR FC.

Mechi hiyo ya jumamosi Rayon Sports itanolewa na Habimana Sosthene koxha msaidizi.

AS Kigali ndiyo inaongoza ligi kuwa muda ikifuatwa na Police FC huko APR FC ikinyemelea katika nafasi ya 3

Christopher Karenzi

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments